Mwanamume mmoja mwenye uume mbili, amezungumza na BBC kuhusu anavyoiishi na hali yake hiyo.
Anajulikana
tu kama 'Triple D,' na ana umri wa miaka 25 kutoka nchini Mashariki mwa
pwani ya Marekani na anadai kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na
wanawake 1,000.
Mwanamume huyu anaugua ugonjwa ujulikanao kama 'Diphallia' ambapo mwanamume anazaliwa na uume mbili.
Kulingana na shirika la kimataifa la afya,BMJ, mwanamume mmoja kati ya milioni tano, duniani huzaliwa na hali hiyo.
ONYO: Taarifa hii ina lugha ambayo kwa baadhio huenda ikawachukiza
"maisha yangu hayatawahi kuwa sawa tena ikiwa nitajitambulisha kwa dunia nzima, '' alisema Triple D.
Hata hivyo BBC ilikubali kubana jina lake na hata kutoonyesha sura yake.
Anasema hataki kuwa kichekesho kwa jamii hasa anakoishi.
Katika siku za uchanga wake, wazazi wake walimwambia kutokana na maumbile yake , yeye alikuwa mtoto mwenye maumbile ya kipekee.
Anakumbuka
wazazi wake wakimketisha chini na kuanza kumuelezea kwamba asidhubutu
kucheza mchezo wa 'kalongo' na watoto wenzake na wala asidhubutu kuvua
nguo zake za ndani mbele ya watu wengine.
'Mawaidha ya wazazi'
Kutokana
na mawaidha ya wazazi wake, aliweza kuweka hali yake kama siri kubwa
sana, lakini alipokuwa katika shule ya upili wanafunzi wenzake
waligundua siri hio na hapo anasema alipitia masaibu si haba.
''Mwanzoni, sikutaka watoto wengine shuleni kujua hali yangu kwani sikutaka kumuudhi yeyote. ''
Natamani sana wazazi wangu wangeniambia na kunitahadharisha kuwa watu huchekelea kitu wasichokielewa.
''Sikutaka
wanaume wenzangu kuhisi vibaya kwamba hawana uume mbili kama mimi na
kuanza kunionea kijicho, au kuanzia kunifanyia stihizai na kunichekelea
kwamba mimi sio mtu wa kawaida'' alisema 'Triple D'.
Alipokua na
umri wa miaka 16, alitaka kufanyiwa upasuaji na kuondolewa uume mmoja
kwa sababu watu hasa wasichana walianz akunitazama sana katika sehemu
yangu ya siri.
''Natamani sana wazazi wangu wangenishauri kuhusu hali yangu basi nisingeopa gata kidogo.''
Alijohiwa
kwa nini ni rahisi kwake kuzungumzia hali yake wakati akiendelea kubana
jina lake? Alijibu na kusema kila mahali ninapokwenda, kila mtu
atanifahamu na kuwa na matarajio makubwa kwangu.
Triple D
amechapisha kitabu kwa jina: ''Double Header: My Life With Two
Penises'', yaani maisha yangu na uume mbili pamoja na anavyokabiliana na
hali yake.
Anasema sehemu zake hizo zinafanya kazi vyema na kwamba
hajabahatika kuwa na uhusiano wa kimapenzi uliodumu kwa muda mrefu.
Kwake changamoto kubwa ni kununua nguo zake za ndani.
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951