Padre Joseph Mabula Mayunga enzi za uhai wake akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza |
Mwili wa Padre Joseph Mabula Mayunga aliyefariki
dunia January 17 mwaka huu katika
hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza leo umewasili katika Parokia ya Mwadui
ambayo aliihudumia kwa muda mrefu enzi za uhai wake.
Mwili huo umewasili katika parokia hiyo ili kutoa nafasi kwa
waamini wa parokia hiyo kutoa heshima zao za mwisho.
Waumini hao wa parokia ya Mwadui pia wameshiriki
misa takatifu ya kumwombea marehemu ambayo imeongozwa na paroko wa parokia ya Sayusayu na Gambela wa seminari ya Awali ya Sayusayu padre Martin Mihango.
Kesho Alhamis mwili wa marehemu Padre Mayunga utapelekwa
parokia ya Buhangija mjini Shinyanga ambapo pia amewahi kufanya kazi enzi za uhai wake ili
kutoa fursa kwa waamini wa parokia hiyo kutoa heshima zao za mwisho na baadaye
kushiriki misa maalumu ya kumwombea.
Padre Mayunga ambaye amefanya kazi katika parokia
mbalimbali za jimbo la Shinyanga ikiwemo parokia ya Mwadui na Buhangija,amefariki dunia katika hospitali ya rufaa ya Bugando alikokuwa
akitibiwa kutokana na kuugua maradhi ya shinikizo la damu na kisukari.
Mazishi ya Padre Mayunga yanatarajiwa
kufanyika siku ya Ijumaa terehe 23,2015 katika makaburi ya mapadri yaliyopo katika Kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.
Mazishi hayo yatatanguliwa na misa ya kumwombea
itakayoongozwa na askofu mkuu wa jimbo kuu la Mwanza na msimamizi wa kitume wa
jimbo katoliki la Shinyanga mhashamu Yuda Thadeus Ruwaich.
Uongozi wa Malunde1 blog unawapa pole ndugu,jamaa na marafiki wote waliofikwa na msiba huo.
Mungu aiweke mahali pema mbinguni roho ya marehemu
Padre Joseph Mabula Mayunga. amen!
Na Simeo Makoba-Shinyanga
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951