KUHUSU KIGOGO ALIYELIPUKIWA BOMU KITANDANI HUKO SINGIDA

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Singida, Thobias Sedoyeka


MKURUGENZI Mtendaji wa Wilaya (DED)
 ya Iramba,mkoani Singida Halima Mpita (47) amenusurika kifo baada ya kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa bomu la kutengenezwa kienyeji.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema mjini hapa jana kuwa tukio hilo lilitokea Januari 2, mwaka huu saa 1.15 asubuhi wakati mkurugenzi huyo akiwa nyumbani kwake, akijiandaa kwenda kazini huku bahasha yenye mlipuko ikiwa juu ya kitanda.

Akisimulia mkasa huo, Kamanda Sedoyeka alisema Desemba 30 mwaka jana saa 4.00 asubuhi, mkurugenzi huyo alipokea bahasha kutoka kwa katibu muhtasi wake na alipoifungua alikuta ujumbe usemao: “Poleni sana, hatuwezi kufanya ‘dili’ la milioni 90 halafu mkala peke yenu, sisi katudhulumu tukawaacha”.

Alisema kuwa baada ya kusoma ujumbe huo, Mpita aliamua kwenda na bahasha hiyo nyumbani kwake, bila kujua iwapo kulikuwa na kitu kingine ndani yake.

“Ilipofika siku ya tukio (jana), akiwa anajiandaa kwenda kazini huku ile bahasha ikiwa juu ya kitanda chake tayari kuichukua, alishitukia ikilipuka kwa kishindo,” alisema Kamanda Sedoyeka.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, mlipuko huo ulitoboa godoro kiasi cha nusu inchi kwenda ndani na upana wa inchi mbili.

Alisema kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kutokana na mlipuko huo, lakini jeshi la polisi likishirikiana na wataalamu wa milipuko kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanashughulikia suala hilo.


Habari kwa hisani ya www.habarileo.co.tz

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post