Afisa afya nchini humo Alex Albertini, amesema wanaamini kuwa kilevi hicho cha kienyeji kilichotengenezwa kwa mtama na mahindi kilikuwa na sumu na kuna hatari ya vifo kuongezeka kutokana na kukosekana kwa vifaa huku watu 196 wakiripoti Hospitali kupatiwa matibabu.
Uchunguzi wa Polisi umegundua kwamba pombe hiyo ilikuwa imewekwa sumu ya nyongo ya mamba na kusema wale waliokunywa wakati wa asubuhi hawakuwa na dalili zozote wakati wale waliokunywa mchana waliugua na wengine kufariki.
Mwanamke aliyetengeneza pombe hiyo pamoja na ndugu zake nao walifariki.
Sample ya damu za watu waliofariki imepelekwa Maputo kwa ajili ya vipimo huku Serikali ikitangaza maombolezo ya siku tatu kutokana na tukio hilo.
Social Plugin