AJALI YA NOAH YAUA WATANO AKIWEMO MJAMZITO,TAIRI LA NYUMA LILIPASUKA

NB-Picha haihusiani na habari hapa chini


Watu  watano  wamefariki dunia akiwemo dereva wake  baada ya gari waliyokuwa wamepanda aina ya Noah kupasuka tairi la nyuma  na kuacha njia hivyo kusababisha vifo vya watu hao katika eneo la Fukayosi  katika Tarafa ya msata wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

 Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari namba T 252 DCB aina ya Toyota Noah lililokuwa likiendeshwa na Ramadhana Masapala (32) lilikuwa likitokea kwenye kituo cha afya cha Miono kuelekea hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda Matei alisema kuwa ndani ya gari hiyo alikuwepo mama mjamzito aliyekuwa akipelekwa hospitali Shukuru Jaba (30) na muuguzi wa kituo cha afya cha Miono Mariamu Omary ambao wao walijeruhiwa.

Alisema wote waliofariki dunia walikuwa ni wakazi na wakulima wa Miono na kuwa  miili ya marehemu hao imepelekwa hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo huku majeruhi wawili wakipelekwa kituo cha afya cha Miono huku mama mjamzito akiandaliwa kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Via>>ITV 

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka  
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post