Afisa
mmoja wa mamlaka ya usafirishaji nchi kavu na majini (SUMATRA) mkoani
kilimanjaro amenusurika kipigo kutoka kwa abiria baada ya kuchana
kibali cha mabadiliko ya ratiba ya bus la Ibra Line walilokuwa
wakisafiria toka moshi kwenda dar badala ya arusha kwenda Dar na
kulizuia lisiendelee na safari kwa madai ya kukiuka ratiba.
Vurumai hiyo ilitokea katika eneo la njiapanda baada ya afisa huyo
ambaye jina lake halikuweza kupatikana kuchana kibali cha mabadiliko ya
ratiba ya bus hilo bus hilo la kampuni ya ibra line lenye namba za
usajili t 288 CDV na abiria hao kuja juu wakitaka waendelee na safari.
Abiria hao wamesema, sumatra hawakuwa na sababu za msingi za
kuchana kibali hicho ambacho kimetolewa na afisa wa usalama barabarani
mkoani k'njaro kwa dharura na kuwachelewesha safari yao kwa kuondoka saa
sita mchana badala ya saa mbili asubuhi.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo bw ibrahimu shayo amesema, BUS hilo
liliharibika wakati likiwa njiani kwenda arusha na kufanyiwa
matengenezo mjini moshi na asubuhi yake lililazimika kuanzia safari yake
moshi badala ya arusha baada ya kupata kibali hicho kutoka kwa mkaguzi
wa usalama barabarani mkoani kilimanjaro.
Afisa wa sumatra mkoani kilimanjaro bw tadey mwita amesema,bus hilo
lilizuiliwa njiapanda ili kupata ushahidi wa ukiukwaji wa ratiba na
kuliruhusu bus hilo liendelee na abiria wake saa sita kasorobo mchana
katika eneo la makao makuu ya sumatra mjini moshi wakati suala hilo
likifanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.