Vyombo
vya habari kutoka Taiwan vimeandika story hii ambayo ni majonzi
makubwa, mtu mmoja amefariki katika mazingira ambayo sio rahisi
kutegemewa kutokea.
Michezo ya kwenye computer ambayo humpa nafasi mchezaji kucheza online ni maarufu sana Taiwan, watu wengi huipendelea kwa sababu ya unafuu wa gharama pia za mchezo huo.
Hsieh amefariki
ndani ya internet cafe baada ya kupata ghafla tatizo la moyo, hiyo ni
kutokana na ripoti ya Hospitali, camera za CCTV zinamuonyesha kuwa
alikaa kucheza game hiyo kwa saa 72, sawa na siku tatu mfululizo.
Wahudumu wa cafe hiyo wamesema ilikuwa kawaida ya Hsieh
kucheza game kwa muda mrefu, akichoka huwa analaza kichwa kwenye meza
hivyo hata wakati amefariki walihisi kwamba amelala kama kawaida yake.
Huyu anakuwa mtu wa pili kufariki kwenye
internet cafe, wa kwanza alifariki New Taipei baada ya kucheza game kwa
siku tano mfululizo.
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951