AFARIKI KWA KUNASWA UMEME AKIIBA NYAYA ZA UMEME HUKO KISHAPU

Ukosefu wa ajira mara nyingi umekuwa ukitajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazowafanya watu wengi kujihusisha na uhalifu na hali ambayo inasababisha baadhi yao kupoteza maisha.

 
Hali hiyo imemkuta Mwanamme Masanja Jilala(38) mkazi wa Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambaye amefariki dunia baada ya kunaswa na nyaya za umeme wakati akijaribu kuiba nyaya hizo.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Longinus Tibishubwamu amesema tukio hilo limetokea jana saa moja na dakika 15 asubuhi katika kijiji na kata ya Mwadui –Luhumbo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Anasema mwanamme huyo alifariki dunia baada ya kunaswa na nyaya za umeme wakati akijaribu kuiba nyaya hizo aina ya Copper zilizokuwa zimechimbiwa ardhini.
Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527