POLISI WATUMIA MABOMU NA RISASI ZA MOTO KUSAMBARATISHA WAENDESHA BODABODA HUKO GEITA


Waendesha bodaboda wakiwa nyumbani kwa mfanyabiashara Joseph  Juma anayedaiwa kuwa amekuwa  akiwatumia vijana  kupanga njama mbalimbali za kuiba pikipiki na wakati mwingine kutekeleza mauaji kwa waendesha bodaboda jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi wa Mkoa wa Geita-picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita



Waendesha bodaboda wakiwa nyumbani kwa mfanyabiashara Joseph  Juma -picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita


Waendesha bodaboda wakiwa nyumbani kwa mfanyabiashara Joseph  Juma-picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
 Awali Bodaboda wakielekea nyumbani kwa mtuhumiwa kuchoma moto nyumba yake-picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Jeshi la polisi Mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya waendesha pikipiki (BODABODA), baada ya kuzingira nyumba ya mfanyabiashara anayesadikiwa kuwa ni mwizi wa pikipiki na kutaka kuichoma moto.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wameimbia Malunde1 blog kuwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Joseph (36) mkazi wa Msalala Road, akiwa amembeba abiria wake Saada Nasorwa (37), walizingirwa na waendesha pikipiki wakitaka kuwachoma moto.

Tukio hilo limetokea jana saa mbili asubuhi, katika maeneo ya NMB Bank ambapo watu hao walikuwa wanaendesha pikipiki yao yenye namba T 234 AVH aina ya sanlg kuelekea makao makuu ya polisi Mkoa.

“Sisi tumewaona watu hawa wakipita hapa wakiwa wamebebana lakini muda mfupi baadaye tuliona waendesha bodaboda wakiwafukuzia huku wakisema ni wezi, wakamatwe, wachomwe moto, wametuchosha kutuibia pikipiki na kuwaua wenzetu,”walisema mashuhuda hao.

Inaelezwa kuwa mfanyabiashara huyo Juma amekuwa akiwatumia vijana  kupanga njama mbalimbali za kuiba pikipiki na wakati mwingine kutekeleza mauaji kwa waendesha bodaboda jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi wa Mkoa wa Geita.

“Taarifa nyingi za huyu jamaa ziko polisi lakini tunashangaa kila akikamatwa anaachiwa huru na kurudi uraiani na kutusumbua sisi wananchi kwanini asifungwe? Na wakati ushahidi tunapeleka yeye ni nani?”alihoji Masanja ambaye ni mwendesha bodaboda.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa amejisalimisha katika kituo chake ili waendesha pikipiki hao wasimuue na kwamba mali zake zote zilizokuwa katika soko kuu la Geita zimeharibiwa vibaya na nyingine kuibiwa.

Hata hivyo kamanda Konyo, aliwataka waendesha bodaboda hao kuwa watulivu wakati jeshi lake likiendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na kuwataka wananchi wenye taarifa na hilo wazitoe ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Nawaomba waendesha pikipiki wote muwe watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na tunaomba wenye taarifa na hili watupe ushirikiano ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani,”alisema Konyo.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527