MSHINDI WA BIG BROTHER AFRIKA 2014,IDRIS AONYWA KUHUSU WANAWAKE WA BONGO

Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan akipozi na mdada.

MSHINDI wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan ameonywa na mashabiki kuwa makini na akina dada kwani mamilioni ya shilingi alizokuja nazo zitawafanya wampapatikie kwa lengo la kumchuna.

Wadau mbalimbali waliokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Jumatano hii kumsubiri wakati akiwasili kutokea Johannesburg, Afrika Kusini, walisema umaarufu na pesa alizonazo utamfanya kuwa kimbilio la masista duu.

“Milioni 510 ni pesa nyingi sana kwa kijana mdogo kama Idris, akijilegeza na kuziona nyingi, muda si mrefu tutasikia hadithi tu, isije ikawa kama yule mwingine nani sijui yuko wapi siku hizi,” alisema Skata Malcom, akimuulizia aliyewahi kushinda shindano hilo miaka ya nyuma, Richard Bezuidenhout.

Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.

 “Mademu wa mjini hawana mchezo, watamlegezea na kuanza kumsifu utafikiri hakuwahi kuishi hapa, kila mmoja atajifanya anamjua, namsihi kama mdogo wangu atulize kichwa ajue kitu cha kufanya, hizi ni hela nyingi kuweza kutimiza ndoto zake, lakini akicheza tu, zitaondoka huku anaziona,” alisema mdau mwingine aliyejifahamisha kuwa shabiki wa kutupwa wa Idris, Jeniffer Radi. 

Idris aliyetegemewa kuwasili Jumatano jioni, alishinda shindano hilo baada ya kukaa katika mjengo huo kwa muda wa siku 63 na hivyo kuwa Mtanzania wa pili kushinda shindano hilo. Richard alipewa kitita cha dola laki moja mwaka 2007.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post