Kumekucha!!! HUYU NDIYO MREMBO WA DUNIA NZIMA SHINDANO LA "MISS WORLD 2014"

Miss World 2014,Rolene Strauss kutoka Afrika Kusini
Miss World 2014,Rolene Strauss akiwa  mwenye furaha kubwa mara baada ya kutwaa taji hilo jioni hii katika ukumbi wa mikutano na maonesho wa ExCel London Exhibition and Convention Centre huko nchini Uingereza.
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Miss World, Julia Evelyn Morley akimtangaza Miss World 2014 ambaye mwaka huu anatokea nchini Afrika Kusini,Rolene Strauss.
Miss World 2014,Rolene Strauss akipunga mkono mara baada ya kutwaa taji hilo.
Mwakilishi wa South Africa, Rolene Strauss amefanikiwa kuvuka hatua zote na hatimaye kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014, nafasi ya pili ikishikwa na Miss Hungary, Edina Kulcsar na nafasi ya tatu kushikwa na Miss USA, Elizabeth Safrit.

Mambo ya Miss World 2014.
Miss World 2013 Megan Young akimvisha Miss South Africa Rolene STRAUSS shashi la ushindi wa mwaka 2014 katika ukumbi wa mikutano na maonesho wa ExCel London Exhibition and Convention Centre. Jumla ya washiriki 125 walipanda jukwaani na kushindania taji hilo, akiwemo mrembo Happiness Watimanywa wa Tanzania. 
Warembo walioshiriki Fainali za 64 za shindano la urembo la Miss World lililofanyika usiku huu jijini London


Leo December 14 kwenye Historia ya mwaka 2014, Mashindano makubwa ya Miss World 2014 yalikuwa yakifanyika London, Uingereza ambapo washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Tanzania, Happiness Watimanywa akiwa mmoja ya washiriki hao.
Mpaka leo asubuhi matokeo ya kura ambazo zilikuwa zikipigwa na watu zilimuweka mwakilishi huyo kuwa katika nafasi ya pili, akitanguliwa na Miss Thailand ambapo iwapoHappiness angekuwa namba moja basi ilikuwa moja kwa moja aingie kwenye Top 10 ya mashindano hayo.
Kutokana na Hapiness kupitwa kura na Miss Thailand hakufanikiwa kuingia kwenye Top 10, huku katika wale waliotajwa ni wawakilishi wawili pekee, mmoja wa South Africa na mwakilishi wa Kenya waliofanikiwa kuingia Top 10.

Mwakilishi wa South Africa, Rolene Strauss amefanikiwa kuvuka hatua zote na hatimaye kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014, nafasi ya pili ikishikwa na Miss Hungary, Edina Kulcsar na nafasi ya tatu kushikwa na Miss USA, Elizabeth Safrit.

Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post