Hot News!! WAVAMIWA WAKIENDA HARUSINI,BASI LAO LATOBOLEWA KWA MISUMARI ILIYOTEGWA BARABARANI


Habari tulizozipata kutoka Kenya ni kwamba maafisa wa usalama katika eneo la Witu katika kaunti ya Lamu mkoa wa Pwani wameanzisha msako wa kusaka genge la watu lililokuwa limevamia basi la abiria lililokuwa likielekea Lamu.Inaelezwa kuwa magurudumu ya basi hilo lililokuwa likitoka Malindi likipeleka watu harusini huko Lamu yalipasuka baada ya kukanyaga misumari iliyokuwa imetegeshwa barabarani na genge hilo.

Dereva alilazimika kulisimamisha basi hilo ambapo jamaa hao waliokuwa na silaha walilivamia lakini hawakujeruhi mtu yeyote na kwenda zao.

Kisa hicho kimetokea katika eneo la Mwisho wa Lami leo majira yaa saa tisa mchana.

Aliyekuwa inspekta mkuu wa polisi David Kimaiyo aliweka marufuku ya kutoka nje katika eneo la Lamu kutokana na ripoti za kijasusi kuwa eneo hilo liko katika hatari ya kuvamiwa na magaidi.

Shirika la utetezi wa haki za binadamu la Muhuri liliwasilisha kesi ya kupinga marufuku ya kutoka nje katika kaunti ya Lamu kesi hiyo itaendelea siku ya Jumanne.


Na Faiz Musa-Malunde1 blog Kenya

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post