Hatarii_ WATU 8 WANUSURIKA KUFA BAADA YA GARI LA MIZIGO KUGONGA NYUMBA WAKIWA WAMELALA NDANI

Watu zaidi ya 8 wamenusurika kifo wakati wakiwa wamelala nyumbani mwao  mtaa wa Heri manispaa ya Tabora, baada ya gari la mizigo aina ISUZU kuparamia nyumba yao, lilipomshinda dereva alipokuwa akikata kona, ambapo mama mjamzito aliyenusurika amekimbizwa hospitalini akiwa na hali mbaya kutokan a na mshituko na hali yake ya ujauzito.

Mashuhuda wa ajali hiyo walioharibiwa thamani zao mbali mbali wamesema kuwa, umefika wakati serikali kubadili adhabu za madreva wazembe ambao wanaendesha vyombo vya usafiri bila kuzingatia sheria zilizowekwa na serikali huku wakipoteza maisha ya wananchi na mali zao.
 Akizungumza juu ya ajali hiyo na kubaini uzembe wa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili t 396 AGS, ambaye hakupatikana mara moja, kamanda wa polisi mkoani tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda aliyefika eneo la ajali hiyo amesema kuwa, mwendesha gari hilo atatafutwa na hatua  stahiki zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha mmiliki wa nyumba hiyo bw.Ramadhani Musa Kaswezi, anayeishi kijijini ilolangulu hakusema lolote akidai kikao cha familia kitatoa maamuzi ili  kuelezea hatua atakazochukua kutokana na wapangaji wake wawili kubolewa nyumba.

Mpenzi Msomaji,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post