Duh!! MAMA HUYU AAMUA KUUA MTOTO WAKE ETI ANAAMINI KUFANYA VILE ATAENDA MBINGUNI

linsey
Mwanamke mmoja nchini Marekani ameamua kumuua mwanae wa kiume wa miaka 10 akiamini ataenda mbinguni na kukwepa matatizo ya dunia.


Mwanamke huyo mkazi wa mji wa Kansas Lindsey Blansett mwenye miaka 33 alifunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya kutenda kosa hilo kwa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Caleb wakati wakiwa nyumbani na dada yake.
caleb
Lindsey Blansett na mwanaye Caleb enzi za uhai wake


Polisi walisema mama huyo alimkata mtoto wake kwa kutumia kisu bila kujali maumivu aliyoyapata na baada ya kutenda kosa hilo aliwapigia polisi simu ili waweze kumshtaki.

Alisema alikua tayari kutumikia adhabu yoyote ile ilimradi ametimiza lengo lake la kumuua mwanaye na kuamini ataenda Mbinguni na kukwepa matatizo ya kidunia ambayo angekutana nayo siku za baadaye.


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527