KUHUSU REKODI YA KWANZA KUTEMBEA JUU YA KAMBA ILIYOVUNJWA BARANI AFRIKA

AVictoria

Unajua Rekodi ya kwanza iliyovunjwa ya watu kutembea juu ya kamba Afrika?

Siku chache baada ya yule jamaa aliyevunja rekodi ya kutembea kwenye kamba umbali mrefu akiwa amefunga macho kwa kitambaa, leo kuna story ya hawa wengine ambao huenda rekodi yao ikawa ya kipekee pia kutokana na mazingira ambayo walifanikisha zoezi hilo.
Safari hii rekodi hiyo imevunjwa Afrika, ambapo Lukas Irmler kutoka Ujerumani naReinhard Kleindl kutoka Austria walifunga safari na kuingia Afrika na kuvunja rekodi hiyo katika maporomoko maarufu ya Victoria Falls yaliyopo mpakani mwa Zambia na Zimbabwe.
0
Unaambiwa wakali hao walimaliza safari yao juu ya kamba umbali wa mita mia moja, ambayo iliisha salama mbali na changamoto ya upepo mkali pamoja na nguvu ya uvutano ya maji ambayo iliwafanya wayumbe lakini kilichowasaidia ni kuangalia mbele muda wote kitu ambacho hakikuwa rahisi.
cegrab-20141109-052515-0-1-362x204
Rekodi hii ni ya pili kuingia kwenye headlines, ambapo ya kwanza ilivunjwa Chicago Marekani na Nik Wallenda ambaye alijifunga kitambaa usoni na kutembea umbali wa mita 182 katika kamba iliyofungwa katikati maghorofa mawili marefu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post