Hili nalo Kubwa!!!WABUNGE WARUKA UKUTA KUINGIA BUNGENI

BOFYA HAPA TUKUTUMIE PICHA ZA VITUKO




Ukweli ni kwamba kuna story ambayo unaweza ukasimuliwa na rafiki yako ama mtu yoyote halafu ukaona kama ni uzushi na hakuna ukweli wowote.


Pata picha pale ambapo Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wanafungiwa geti la kuingia ndani ya Ukumbi Bunge …

Nakupa story kutoka Nigeria, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Aminu Tambuwal amelazimika kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo wa dharura baada ya Polisi kufunga milango ya Bunge hilo kwa sababu za kiusalama.
Spika huyo alijitambulisha kwa Maafisa Usalama hao ili wamruhusu aingie lakini hakuna aliyeonekana kujali ombi lake wala kumjibu, japo baadaye walimruhusu aingie kupitia mlango mdogo wa dharura huku wabunge wengine wakizuiwa kuingia kitendo kilichowafanya waamue maamuzi magumu ya kuingia ndani ya Bunge kwa kuruka ukuta.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nigeria, Suleiman Abba amesema walilazimika kuzuia mtu yeyote kuingia ndani ya jengo hilo na kuweka ulinzi wa hali ya juu baada ya kupata taarifa kwamba kuna majambazi walipanga kuvamia Bunge hilo.

Polisi waliwashambulia kwa gesi ya machozi Wabunge waliokaidi amri ya kutokuingia Bungeni, Wabunge wawili walipoteza fahamu katika vurugu hizo
BOFYA HAPA TUKUTUMIE PICHA ZA VITUKO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527