STAND FC NA NDANDA FC HAPAKALIKI JUMAMOSI,MAANDALIZI YAMEKAMILIKA




Maandalizi ya mchezo kati ya Stand fc ya Shinyanga na timu ya Ndanda fc ya mkoani Mtwara unaotarajiwa kufanyika kesho kutwa katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga yamekamilika kwa asilimia mia moja.


Mjumbe wa kamati ya Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga Mbasha Matutu  milango itafunguliwa saa 6 mchana siku ya Jumamosi ambapo mchezo utafanyika kuanzia saa kumi jioni.

Tayari timu ya Ndanda fc,waamuzi na wasimamizi wote wamesha wasili mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo huo ambao unasuburiwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mpira wa miguu na wakazi wa mkoa wa Shinyanga.

Kiingilio cha mchezo huo ni shilingi elfu tano kwa watu wote na tiketi zitaanza kutolewa kesho Ijumaa katika eneo la Uwanja wa Kambarage,kituo cha mabasi cha zamani na kituo kipya cha mabasi mjini Shinyanga.



Mchezo huo  utakuwa ni mchezo wa ufunguzi wa msimu wa ligi kuu Tanzania ambapo mgen rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.

Na Kadama Malunde-Shinyanga 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post