MASKINI_TAZAMA WANAFUNZI HAWA WANAVYOTESEKA SHINYANGA TENA SHULE MAALUM,VIFAA VYA KUJIFUNZIA VIBOVU,MADARASA YAMECHOKA

Hapa ni kwenye mlango wa moja ya darasa la watoto wenye ulemavu wa macho(Wasioona) katika shule ya msingi Buhangija Jumuishi katika manispaa ya Shinyanga.Wanafunzi wasioona wanaosoma katika shule hiyo wanakabiliwa na changamoto ya  upungufu wa mashine za kujifunzia hali inayoelezwa kuwapa wakati mgumu walimu wanaowafundisha na wanafaunzi kuelewa vyema masomo yao.
Hivi sasa wanafunzi wasioona wapo 38,  wavulana 25 na wasichana 13,lakini mashine za kujifunzia zinazotumika ni 8 pekee kati ya 28 zilizopo.Picha na Kadama Malunde

Moja kati ya mashine 8 nzima kati ya mashine 25 zilizopo,mbovu ziko 20. Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha watoto wenye ulemavu katika kituo hicho Bright Mduma  ameimbia Malunde1 blog kuwa  wamekuwa wakizitengeza mara kwa mara hivyo kuwaomba wadau wa elimu watoto kujitokeza kusaidia watoto hao.Picha na Kadama Malunde
Ndani ya moja ya madarasa lenye wanafunzi wasioona-Pichani ni mwalimu Agnes Makambajeki akiwa na wanafunzi wake wakijifunza kwa kutumia vifaa ambavyo vinaelezwa kuwa ni vibovu.Picha na Kadama Malunde
 Miongoni mwa vifaa vinavyotumiwa na watoto wenye ulemavu kujifunzia katika shule ya msingi Buhangija iliyopo Shinyanga mjini.Picha na Kadama Malunde


Mwalimu Mduma(Kushoto) alisema wana upungufu wa vifaa kwa watoto wasioona,mashine za wasioona( Perking Braillers) nyingi zimeharibika,hata karatasi na kalamu maalum kwa wasioona hazitoshi.Picha na Kadama Malunde
Pichani ni mfano wa kalamu maalum inayotumiwa na wanafunzi wasioona katika shule ya msingi Buhangija mjini Shinyanga.Picha na Kadama Malunde
Mwalimu mkuu msaidizi katika shule ya msingi Buhangija akizungumza na Malunde1 blog ilipotembelea shule hiyo,Pius Lukala ambapo amesema mbali na kuwepo kwa changamoto ya vifaa vya kujifunzia  zikiwemo meza na viti pia walimu wanaofundisha watoto wasioona ni watatu pekee na wanahitajika walimu wawili ili wawe watano wafundishe kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.Picha na Kadama Malunde
 Kushoto ni mwalimu Kwandu Ngalaba akiendelea na darasa.
Picha na Kadama Malunde
Hili ni darasa jingine ambapo watoto wenye ulemavu na wasiokuwa na ulemavu wanasoma pamoja katika shule hiyo.Picha na Kadama Malunde

Mwalimu mkuu wa shule ya Buhangija Peter Ajali akizungumza na Malunde1 blog,ambapoa alisema shule ya msingi Buhangija  Jumuishi iliyopo katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia hivi sasa ina watoto 275, wasioona 38,wasiosikia 49 na wenye ulemavu wa ngozi 188.Alisema
pamoja na shule hiyo kuwa na wanafunzi wenye ulemavu pia wapo wanafunzi wasiokuwa na ulemavu 758.Picha na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post