MAJAMBAZI WAMWIMBIA MSALABA NA PETE ASKOFU WA KANISA KATOLIKI


Kadinali Dom Orani Tempesta 


Watu waliokuwa wamejihami wamemuibia Askofu mkuu wa Rio de Janeiro nchini Brazil msalaba wake na pete

Kadinali, Dom Orani Tempesta, alikuwa njiani kuelekea kuhudhuria mkutano mjini alipovamiwa na majambazi hao.

Mmoja wa majambazi aliyekuwa na bunduki katika kanisa, alimfahamu kadinali huyo na kumuomba msamaha.
Hata hivyo, hilo halikushutua genge hilo ambalo liliendelea kumpora kadinali huyo, na hata nusura wampore gari lake.

Vitu vilivyoibwa vilipatikana baadaye.





Hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyiika Jumatatu jioni katika mtaa wa Santa Teresa.

Mwandishi wa BBC Gary Duffy, anasema kuwa visa vya wizi hutokea mara kwa mara katika mtaa huo wenye shughuli nyingi za kitalii na kwamba visa hivyo vimekuwa vikiongezeka sana mwaka huu.

Mwanafunzi wa dini pamoja na mpiga picha mmoja waliokuwa kwenye gari na kadinali huyo pia waliporwa.

Licha ya tukio hilo, kadinali aliendelea na shughuli zake huku mwanafunzi na mpiga picha wakienda kuripoti kwa polisi.

Pete ya kadinali na msalaba, vilipatikana pamoja na simu yake ya mkononi

Hata hivyo, vifaa vya mpiga picha havijapatikana.

Dom Orani Tempesta alitawazwa kama kadinali na Papa Francis mapema mwaka huu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post