MABASI YA SUPER FEO NA UPENDO YAGONGANA YAKIKWEPA PUNDA BARABARANI


Basi la kampuni ya Super Feo likiwa limegongwa kwa nyuma na basi la 
Upendo leo asubuhi. 

Mabasi yote yanafanya safari kutoka Dodoma kwenda Iringa (upendo) na Super Feo (Songea) .


Taarifa za kutoka eneo la tukio zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni punda aliyekatisha barabarani na  mwendo kasi wa basi la upendo bila umakini wa dereva wa basi hilo.

Abiria waliokuwa katika basi la upendo walisema kuwa  walikuwa wakilifuata basi la Super feo kwa kasi bila kuacha safety distance (nafasi ya usalama kati ya basi moja na lingine nyuma au mbele ) hali iliyopelekea ajali hiyo kutokea pale dereva wa basi la Super feo aliposimama ghafla kuepuka kugonga punda aliyekuwa akikatisha barabarani.

Taarifa zinaendelea kudai kuwa dereva wa basi la upendo amevunjika miguu na wengine wamejeruhiwa vibaya!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post