Breaking news!! SERENGETI FIESTA YASABABISHA MAUAJI SHINYANGA


 Mwili wa marehemu Mussa ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakati wa kufanyiwa postmoterm leo


Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mussa Shija mkazi wa kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa kupigwa kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika akiwa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililokuwa linafanyika usiku wa kuamkia leo katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga

Akizungumza na Malunde1 blog mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi  wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mussa Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kijana huyo aliuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana nje ya fensi la uwanja mdogo wa Kambarage palipokuwa panafanyika tamasha la Fiesta.

Hata hivyo amesema jeshi la polisi litatoa taarifa kamili baadaye kwani linaendelea kufanya uchunguzi


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post