ANGALI PICHA_ BASI LA RUKSA LAUA WAWILI NA KUJERUHI 65 LEO HUKO KIGOMA,LILIKUWA LINATOKA KIGOMA KWENDA KAHAMA

Basi la Ruksa aina ya Scania lenye namba za usajili  T 273 ACX llililokuwa iliktokea mkoani Kigoma kwenda wilayani Kahama mkoani Shinyang'a likiwa limepata ajali katika kijiji cha Kanyonza wilayani Kakonko,mkoani Kigoma ambapo watu Wawili walipoteza maisha papo hapo na wengine 65 kujeruhiwa katika Ajali hiyo ya Septemba 08,2014,majira ya saa Sita mchana

Pichani juu na chini ni Jeshi la polisi wilaya ya Kakonko lilifika eneo hilo na kuwachukuwa waliojeruhiwa  na kuwapeleka katika hospitali ya wilaya  kwa ajili ya matibabu.


Taswira ya Basi hilo la Ruksa likiwa eneo la Ajali ambapo mashuhuda wanasema chanzo cha ajali kilisababishwa na mwendo kasi.

Pichani ni Baadhi ya Majeruhi wa ajali hiyo wakiwa wodini  katika hospitali ya wilaya ya Kakonko kwa ajili ya matibabu.

Picha na Mdau Mwanawamakonda  WhatsApp +255789925630.

BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post