WAHAMIAJI HARAMU ZAIDI YA 10 WAKAMATWA MJINI KAHAMA

Wahamiaji haramu wakiwa ofisi za uhamiaji wilaya ya kahama mkoani Shinyanga baada ya kukamatwa kituo cha basi Kahama
Afisa wa uhamiaji akichukua maelezo kwa mhamiaji haramu Tegemea Benjamini ofisi za uhamiaji Kahama
Irene mkazi wa Ngara ambaye mmoja wa tanzania ambaye anajiushisha na kukaa na wahamiaji haramu na mtoto Khadija (8)mbaye ni raia wa Burundi anayefanya naye kazi kwake.
Baadhi ya wahamiaji haramu wakiwa chini ya ulinzi katika ofisi za uhamiaji Kahama baada ya kukamatwa.
Mtoto Khadija akiwa na mtoto wa Ireni stephen ambaye amembeba kwa ajili ya kumlea mtoto huyo.
Irene akiwa na watoto wake wawili na mfanyakazi wake wa watoto wake Khadija ofisi ya uhamiaji Kahama kwa mahojiano.
Irene akiwa na afisa wa kike ofisi za uhamiaji Kahama na watoto wake baada ya kukamatwa kituo cha mabasi.
Irene akihojiwa na kamishina wa uhamiaji Zakaria Misana ofisi kwake kwa kosa la kukaa na mtoto wa miaka 8 kumfanyisha kazi kinyume na sheria. 
Kamishina wa uhamiaji Zakari Misana akiongea na waandishi wa habari
Wahamiaji haramu wakiwa ofisi za uhamiaji kwa kosa la kuingia nchini bila kibali
Afisa wa uhamiaji akifanya mahojiano na moja wa wahamiaji haramu ofisi za uhamiaji .



Wahamiaji haramu kumi na watoto watatu wamekamatwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga wakiwa wakielekea mkoani Tabora kwenye mashamba ya tumbaku kwa ajili ya kilimo.


Kamishana wa Uhamiaji Wilaya ya Kahama Zakari Misanao alisema wahamiaji hao walikamatwa katika kituo cha mabasi cha Kahama wakati wakimsubiri mwenyeji wao ili kuwapeleka mkoani Tabora.

Alisema kuwa wahamiaji hao ambao ni raia wa nchi ya Burundi waliagizwa na mkazi mmoja wa Tabora aliyejulikana kwa jina moja la Shaba ambaye alikimbia baada ya wenzake kukamatwa.

Misana aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Emily Havyarinana(33),Habimana Paschal(45),Masabo Tadei( 34),Bahati Leopoo( 42),Niondeze John(24),Emmanuel Mathayo( 21),Tegemea Benjamini( 23),Joseph Elias (12), ,Laneck Wilford (17),Estar John (18) raia wa Burundi pamoja na Irene Stephan0(20)raia wa Tanzania mkazi wa Ngara.

Misana alisema kuwa walikuwa wanakwenda Mkoani Tabora katika kijiji cha Isakamleme kwa ajili ya shughuli za kuvuna mahindi, kuchambua Tumbaku pamoja na kuvuna mpunga.

Katika hatua nyingine alisema kuwa Irene Staphano ameajili mtoto mwenye umri wa miaka(8) aliyejulikana kwa jina moja la Khadija mkazi wa Burundi jambo ambalo ni kosa kuajili mtoto mdogo na ni kinyume cha sheria ya Jamhuri ya Muungano waTanzania.

Misana alisema miezi kama hii katika mikoa ya mipakani kumekuwa na tatizo la wahamiaji haramu wanaokimbilia mikoa ya kagera,Tabora pamoja na Shinyanga, ambapo wilaya ya Kahama imejipanga vyema katika kamati ya ulinzi ili kudhibiti jambo hilo.

Misana aliwataka watendaji wa kata na vijiji vilivyopo mipakani kushirikiana na wananchi kudhibiti matatizo ya wahamiaji hao ambapo amesema kuwa atakayebainika kuishi na raia ambaye sio raia ya TanzAnia atachukuliwa hatua kali za kisheria.




Alisema kuwa wahamiaji hao watachukuliwa hatua za kisheria baada ya kuingia nchini bila kibali hivyo watafikishwa mahakamani wilayani humo ili kujibu kesi inayowakabili.


Na Mohab Dominick-Mohab Matukio blog

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post