TAZAMA PICHA_MFANYABIASHARA WA GEITA ATOA GARI LA MIL 10,MSHINDI MISS LAKE ZONE 2014

 Mdhamini wa shindano la Miss Lake zone 2014 LEONARD BUGOMOLA, mkazi wa Mtaa wa Nyamalembo  Wilayani Geita Mkoani hapa ambaye ni Mkurugenzi wa Lenny Hotel, akiwa na Walimbwende 18 akiwaonyesha gari  alilotoa zawadi kwa ajili ya mshindi wa kwanza atakayeibuka kidedea mwishoni mwa mwezi huu. Picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Nani kuondoka na gari hilo kati ya warembo 18 kutoka kanda ya ziwa . Picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

IKIWA ni siku chache wasichana 18 kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wanaoshiriki mashindano ya Taji la Miss Lake Zone  mwaka 2014 kutembelea kituo cha watoto yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mtaa wa Mbugani Wilayani Geita mkoani Geita na kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi laki 350,000/= Mamiss wameendelea kuonekana mfano kwa kufanya usafi katika mji wa Geita.

Wakizungumza na Malunde1 blog Mamiss hao walisema kuwa wameamua kufanya usafi katika mji huo ikiwa ni kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo Omary Mangochie ya kufanya mji kuwa msafi kwa kufanya usafi kila Alhamis .

Mamiss hao  wametoa shukrani zao kubwa kwa mdhamini wao Leonard Bugomola ambaye ametoa vyumba 10 vya kulala ambapo kila chumba ni shilingi 80,000/=   kila siku  na chakula  chenye thamani Tsh 15,000 kwa kila mshiriki huku wakiishi  hotelini kwake kwa siku kumi wakiwa kwenye mazoezi.

Katika namna ya pekee pia ametoa  gari  lenye thamani ya Tshs. Milioni kumi (10,000,000/=) kwa atakaye kuwa mshindi wa kwanza katika shindano la Miss Lake zone 2014.  

Mdhamini huyo Leonad Bugomola ambaye ni mfanya bishara mkoani humo pia mmiliki wa Lenny Hotel alisema kuwa ameamua kutoa zawadi hizo kutokana na Mungu kumjalia alivyo navyo na kuwa na kipaji cha kupenda michezo mbalimbali.

Bugomola aliwaomba wafanya biashara wenzake  wa mkoa wa Geita kujitolea kwa kudhamini Mamiss na kuacha Dhana ya kuwa Umiss ni uhuni kwani Umiss ni ajira kama ajira zingine.

Shindano la kumpata Miss ake Zone litafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu wa nane (8) mbapo mshindi wa kwanza atajinyakulia zawadi ya Gari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post