MADAKTARI HAWA NOMA_ WAUNDA MASKIO NA KUMPA KIJANA ASIYE NA MASIKIO TANGU AZALIWE



Madaktari nchini Uingereza wameumba masikio kutokana na ubavu wa kijana (pichani kulia)aliyezaliwa bila ya viungo hivyo muhimu.

 Kijana huyo wa miaka tisa Kieran Sorkin alizaliwa bila masikio na madaktari wamekuwa wakifanya majaribio ya mbinu mpya ya matibabu katika hospitali ya Great Ormond Street iliyoko jijini London..

Takwimu nchini Uingereza zinaonesha kuwa takriban watoto 100 huzaliwa bila kiungo hicho muhimu nchini Uingereza .

 Madaktari wanaita ugonjwa huo microtia.

 Kieran aliyezaliwa kama kiziwi hakuwa na masikio alipozaliwa badala yake alizaliwa na shimo mbili na ndewe tu badala ya masikio.

 Tayari kieran anasikia baada ya upasuaji wa awali ambao ulimsaidia kupandikiza kifaa kinachomsaidia kupaza sauti ndani ya masikio yake.

 "Ningependa watu wakome kuniuliza kwanini unakaa tofauti hivi ", alisema Kieran akiwa katika mtaa wa Hertfordshire.

 "nimefurahishwa sana kufanana na marafiki zangu ''.

 "Hata mimi ninafurahi kuwa sasa nitaweza kuvaa miwani na vifaa vya kusikizia muziki."



 Mamake Kieran ,Louise Sorkin alisema kuwa kijana huyo ni mchangamfu sana na alikuwa anasubiri kwa hamu kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza masikio hayo.

 "Sikuwa nafurahiwa watoto wenzake wakimkejeli kutokana na maumbile yake."

 Asubuhi ya siku ya upasuaji huo Neil Bulstrode aliumba masikio hayo na akapandikiza akitumia teknolojia ya kisasa ya kushona masikio hayo chini ya ngozi ya kichwa chake .

 Wanasayansi hao wanasema kuwa walitumia mbinu mpya ya kukuza viungo hivyo.

 Kieran alifurahishwa sana alipooeshwa masikio yake mapya siku tatu baada ya operesheni hiyo.
        via>> bbc swahili 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527