Ni katika eneo la ajali |
Hali ni tete sana eneo la Mkolye, takribani km 4 toka Mjini Sikonge baada ya basi la Sabena lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Mwanza na basi la A.M. toka Tabora kwenda Mpanda Katavi kugongana uso kwa uso.
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio
Zoezi la kutoa miili ya marehemu likiendelea
Miili ya marehemu ikiwa eneo la tukio
Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba watu zaidi ya 10 wanadaiwa kupoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 70 wajeruhiwa baada ya basi la linalofahamika kama AM linalofanya safari yake Mwanza mpaka Mpanda kugongana uso kwa uso na basi lingine la Sabena ambalo linafanya safari zake Mbeya kwenda Tabora.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.
Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani Sikonge.
Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papo hapo na kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi (Day-worker)
Inaelezwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibika vibaya sana.
Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la Sabena lililokuokea Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea Mwanza kwenda Mpanda.
Majeruhi baadhi wakiwa wamekatika mikono na miguu,wamepelekwa katika Hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge.
Majeruhi baadhi wakiwa wamekatika mikono na miguu,wamepelekwa katika Hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.