MADAKTARI NCHINI TANZANIA WALAANI VIUNGO VYA BINADAMU KUTUPWA JIJINI DAR ES SALAAM

Chama cha Madaktari nchini Tanzania kimelaani kitendo cha kutupwa kwa viungo vya binadamu nje ya jiji la Dar es Salaam kinyume cha sheria.
Rais wa chama hicho, Dk. Primus Saidia ametaka hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya wahusika ikiwemo kupigwa marufuku kwa mtu au taasisi iliyohusika kuendesha shughuli zozote za utafiti kwa kutumia viungo vya binadamu.

Dk Primus ameweka bayana kwamba, licha ya fani hiyo ya udaktari kuruhusiwa kutumia viungo vya binadamu katika shughuli mbali mbali za utafiti kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kimataifa lakini ameelezea kwamba kitendo hicho kimekiuka haki za binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho cha madaktari hapa jijini Dar es Salaam, kiongozi huyo ametaka hatua madhubuti zikuchuliwe dhidi ya wahusika ikiwemo kufungiwa.

Sakata la kutupwa kwa viungo hivyo kinyume cha sheria katika mji wa Mbweni nje ya jiji la Dar es Salaam siku mbili zilizopita, lilizua taharuki miongoni mwa watu wa kada mbalimbali.

Tayari watu wanane kutoka Chuo cha udaktari cha IMTU kilichopo hapa jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusishwa kwa kutupwa kwa viungo hivyo ambavyo viliwekwa katika mifuko ya plastiki ipatayo 85.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post