Maajabu haya!! MADAKTARI WAGUNDUA MWANAMME YUKO "PERIOD"( Hedhi),WAMKUTA NA MAYAI YA UZAZI YA KIKE

Ajabu: Madaktari wagundua mwanaume yuko kwenye
Maajabu yanaendelea duaniani, wiki hii tuliandika habari kutoka China iliyohusu kijana aliyeng’olewa meno 132, lakini pia kuna habari nyingine kutoka nchini humo ambayo imewaacha wengi midogo wazi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Shagalist, mwanaume aliyetajwa kwa jina la Mr. Chen, mwanandoa mwenye umri wa miaka 44 na mkaazi wa Zhejiang, China amegundulika kuwa alikuwa katika siku zake kama inavyokuwa kwa wanawake  kwa mzunguko wa hedhi(period) baada ya kufika hospitali akilalamika sana kuwa na maumivu ya tumbo.
Taarifa zilizotolewa na madaktari wa hospitali ya Yongkang zinaeleza kuwa mwanaume huyo alifanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa alikuwa na mfumo wa uzazi wa mbegu za mwanamke ingawa alikuwa na uume.
Ingawa mwanamme huyo aliwaeleza madatari kuwa amekuwa akishiriki na mkewe tendo la ndoa kwa miaka kumi ya ndoa yao bila tatizo, madaktari hao waligundua kuwa alikuwa anatoa mkojo wenye damu ambao uliwasababisha wafanye uchunguzi wa kina na kugundua hali hiyo.
Msemaji wa hospitali hiyo alieleza kuwa vipimo vya ACT Scan vilionesha wazi kuwa alikuwa na uterus na ovaries (mayai ya uzazi), na kwamba madaktari walieleza kuwa alikuwa amechelewa kupata matibabu kwa tatizo lake hilo lisilo la kawaida.
Mr. Chen mwenyewe alieleza kuwa  alikuwa anasikia dalili ya vitu vingi visivyo vya kawadia hata katika maumbile yake, na kibaya zaidi ni pale alipoanza kuona anatoa damu badala ya haja ndogo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post