KAMANDA KOVA ATOBOA SIRI YA BENKI NYINGI KUVAMIWA NA MAJAMBAZI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjau4kOkoAjCPP_AOoPlHvpYZx7KrkFQvxm_ermxKDQ-znCZX34mxsPt_1qxxM6uvC7FqtpBO01kavZ5UVMuE82sbuBuo2XkXjQ4Af-UGdLya674A50QCCY0NBgcKVAputwmKVpBgujzpH/s1600/3.jpg
Kamishina wa polisi kanda maalum ya Daresalaam Suleimani Kova akitoa ufafanuzi jambo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Jijin Dar es Salaam.


 JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefichua siri ya kuongezeka kwa vitendo vya  ujambazi katika Benki mbalimbali hapa nchini na kusema vitendo hivyo vinasababishwa na wamiliki wa benki hizo kulipuuza jeshi la polisi pale linapowapa ushauri.

Kauli hiyo ya jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam imekuja  ikiwa ni siku moja kupita baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kuvamia katika Benki ya Stanbic tawi la Kariakoo lililoko mtaa wa Swahili na kukomba mamilioni ya pesa aliyokuwa nayo mteja.

Kauli hiyo imetolewa muda mfupi uliopita na kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,ambapo alisema watu wanaochangia vitendo hivyo vya ujambazi kuzidi kuongezeka katika benki mbalimbali hapa nchini ni wamiliki wa benki kupuuza ushauri wa jeshi la polisi.

Ushauri wa jeshi la polisi ni ule uliowataka waache kutumia walinzi wa makampuni binafsi peke yake hivyo watumie na walinzi kutoka jeshi la polisi.

 “Nataka niwambie waandishi hivi vitendo vya uvamizi kwenye mabenki vinatokana na wamiliki wa mabenki hayo kupuuza ushauri wetu uliowataka kwenye shughuli za ulinzi kwenye mabenki watumike polisi tu,lakini wao wakapuuza,ukitaka kuamini nenda kwenye mabenki yanayolindwa na polisi kama utaona kama kuna uvamizi wowote unaotokea,kwa sababu majambazi hao wanashindwa kuvamia kutokana na umakini wa jeshi la polisi”alisema Kova

Kamishna Kova,alisema kwa sasa jeshi la polisi limejipanga kuongea na Benki kuu ya Tanzania (BOT) ambaye ni kiongozi wa benki zote hapa nchini na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili  la benki zingine kupuuza ushauri huo wa jeshi la polisi.

Aliongeza kuwa jeshi hilo la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, limeanza msako mkali wa kuwatafuta majambazi watano waliovamia jana majira ya mchana kwenye Benki ya Stabinc Tawi la Kariakoo lililoko mtaa wa Shwahili .

  Kwa Mujibu wa Kamishna Kova alisema watu watatu kati yao waliingia ndani ya benki hiyo wakiwa na mifuko mikubwa wakijifanya ni wateja wanapeleka fedha nyingi katika benki hiyo, na watu hao walipoingia ndani walianza kuwalazimisha kuvuka wigo wateja wa kwaida na kutaka kuingia kwa nguvu kupora fedha.

Lakini kutokana na benki hiyo ya Stabinc kuwa na mitambo ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na ving'ora vya tahadhari,ikasaidia kwa majambazi hao kushindwa kuingia ndani kuiba pesa za benki hiyo kutokana na ving'ora hivyo kupiga kelele na kuanza kuwapa uwoga majambazi hao ,ambapo walifanikiwa kuiba pesa za mteja mmoja ambaye alikuwa anataka kuweka pesa kwenye benki hiyo.

 Kova alisema majambazi hao walipotoka nje ya benki hiyo walipiga risasi juu ili kuwapa hofu wananchi waliokuwa nje ya benki hiyo,ambapo kwa mujibu wa kamishna Kova anasema bado wanaendelea kuwafuatilia majambazi hao.

Katika hatua nyingine jeshi hilo la polisi limejipanga ipasavyo kwenye sikukuu ya IDD El Fitr 2014,ambapo jeshi hilo limesema limepanga kushikirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na kikosi  cha zima moto na uokoaji,kampuni binafsi za ulinzi lengo ni kuhakikisha wananchi wanafurahia kwa utulivu na amani kwenye sikukuu hii.

via>>matukiotz

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527