![]() |
| Maandamano yanaendelea watoto wa shule za msingi,sekondari,taasisi,asasi na wadau mbalimbali wa haki za watoto wakiwemo waandishi wa habari walikuwepo |
![]() |
| Wakati wa maandamano |
![]() |
| Watoto wakiimba kwaya katika viwanja vya shule ya msingi Mapinduzi A muda mfupi baada ya mgeni rasmi naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu David Nkulila kupokea maandamano hayo |
![]() |
| Watoto wakionesha shughuli wanazofundishwa na shirika la Compassion kwa mgeni rasmi |
![]() |
| Mkurugenzi wa Compassion kituo cha AICT Ngokolo bwana Peter Joshua akimwongoza mgeni rasmi David Nkulila ambapo alisema compassion inafundisha pia watoto kuhusu namna na kutumia vyombo vya muziki kama unavyoona pichani mtoto anacheza na vyombo utafikiri alizaliwa navyo |
![]() |
| Watoto wakicheza katika viwanja vya shule ya msingi Mapinduzi A mjini Shinyanga |
![]() |
| Wadau wa haki za watoto wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani hapo |
![]() |
| Wadau wa haki za watoto wakisikiliza risala ya watoto |
![]() |
| Watoto wakifanya yao katika viwanja vya shule ya msingi mapinduzi A jana mjini Shinyanga |
![]() |
| wakili paroko kanisa katoliki parokia ya Shinyanga mjini jimbo la Shinyanga padre Joseph Okuruti akibariki kaburi la mtoto Rose aliyeuawa mwaka 2013 siku ya mtoto wa Afrika |
![]() |
| Kaburi la mtoto Rose Dotto aliyeuawa kikatili kwa kupigwa kitu kizito kichwani kisha mwili wake kutupwa jalalani siku ya mtoto wa Afrika mwaka 2013 |
Soma hapa chini Habari kamili---
Watoto katika manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali
kutoa elimu ya kutosha inayohusu sera na haki za watoto ili watoto waweze
kutambua haki zao za msingi katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili
ikiwemo ukatili na unyanyasaji.
Wito huo umetolewa jana na mwenyekiti wa baraz la
watoto katika kata ya Ngokolo Anitha
Joseph ambaye pia ni mwanafunzi wa shule ya msingi Mapinduzi A katika manispaa
ya Shinyanga wakati akisoma risala kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa
Afrika yaliyofanyika katika shule ya Mapinduzi A katika manispaa hiyo.
Akisoma risala hiyo alisema matukio ya unyanyasaji na
ukatili dhidi ya watoto unachangiwa na watoto kutojua haki zao huku jamii nayo
ikiwa haielewi chochote matokeo yake kila kukicha ukatili,unyanyasaji unazidi
kujitokeza katika jamii.
“Tunaiomba serikali na wadau mbalimbali kutoa elimu ya
kutosha inayohusu sera na haki za mtoto kwa jamii yetu na wakazi wa manispaa ya
Shinyanga,kwani tunanyanyasika,pia tunaiomba serikali yetu iwachukulie hatua
wote wanaokiuka na kuvunja upatikanaji wa haki ya mtoto kupata elimu
bora”,alisema Anitha.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa watoto alisema
miongoni mwa vikwazo katika sekta ya elimu ni pamoja na jamii kuwa na uelewa
mdogo kuhusu elimu hali inayosababisha watoto kukosa elimu bora kutokana na
vikwazo wanavyovipata mfano baadhi ya jamii kuwanyanyasa watoto wa kike kwa
kuozesha katika umri mdogo badala ya kuwasomesha.
Akizungumza katika maadhimisho hayo mgeni rasmi naibu
meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila alisema manispaa ya Shinyanga bado
inakabiliwa na ukatili dhidi ya watoto na sasa limezuka wimbi la wazazi na
walezi kukwepa kulea watoto kwa visingizio mbalimbali kama vile kudai kuwa wana
hali ngumu kimaisha.
Nkulila alisema wazazi na walezi wamekuwa wakikwepa
kulea watoto na kuanza kuilalamikia serikali iwatendee haki wakati wanakwepa
majukumu yao kama walezi wa watoto.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa
ya Shinyanga yameanza kwa maandamano kisha misa ya kumwombea mtoto Rosemary
Dotto Peter(12) aliyeuawa kikatili kwa kupigwa kitu kizito kichwani kisha mwili
wake kufungwa kwenye boksi kisha kutupwa kwenye jalala la takataka eneo la
Ngokolo mjini Shinyanga mwaka 2013 siku ya mtoto wa Afrika.
Misa ya kumwombea mtoto Rosemary imefanyika katika
makaburi ya Majengo mjini Shinyanga alikozikwa na kaburi lake kujengwa na
manispaa ya Shinyanga kama kumbukumbu,ambapo misa hiyo imeongozwa na wakili
paroko kanisa katoliki parokia ya Shinyanga mjini jimbo la Shinyanga padre
Joseph Okuruti.
Na Kadama Malunde- Shinyanga
















Social Plugin