Kuna habari imetapakaa katika mitandao ya kijamii kuwa waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi wa Tanzania mh. Shukuru Kawambwa amefariki dunia....
Huu hapa ndiyo ukweli wa habari hii,kama mtandao huu wa Malunde1 blog ulivyoahidi kukutaarifu kuhusu ukweli wa habari hiyo,ambayo kiukweli malunde1 blog ilipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.
TAARIFA YA KANUSHO HII HAPA
Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.
UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.

Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze
Mbunge -Chalinze
Social Plugin