JAMAA ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUSEMA "HAMWAMINI MUNGU"

Mubarak Bala
Mwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini NIGERIA.

Duru katika hospitali hiyo zimesema kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa kwa matatizo ya kiakili na kwamba ataendelea kuzuilikwa kwa muda mrefu.

Mubarak Bala alizuiliwa kinyume na matakwa yake hospitalini baada ya familia yake kumpeleka huko kwa matibabu.

Jimbo la Kano lina idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu, na limekuwa chini ya sheria za kiisilamu tangu mwaka 2000.

Shirika hilo la kimataifa limesema kuwa wakati ambapo Bala aliwaambia jamaa wake kuwa hamuamini Mungu, familia yake ilimpeleka kwa daktari kuuliza ikiwa akili yake iko timamu.
Licha ya kufahamishwa kuwa mwanamume huyo hana tatizo lolote la kiakili, familia ya Bala ilitafuta ushauri wa daktari mwingine aliyewafahamisha kuwa hatua yake ya kumkana Mungu, inatokana na matatizo ya kiakili.

Bwana Bala, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu, alilazimishwa kupata ushauri wa daktari wa kiakili , ingawa alitumia simu kuwasiliana na wanaharakati wa haki za kibinadamu.

Hospitali ambako alikuwa ana pokea matibabu ilisema katika taarifa yake kuwa Bwana Bala hana tatizo lolote la kiakili na kuwa yuko sawa.


Alilazwa hospitalini kwa sababu alihitaji kuchunguzwa na daktari, ilisema taarifa ya hospitali hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527