Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HUYU NDIYE REFA WA KOMBE LA DUNIA ALIYEINGIA MATATANI BAADA YA KUSHANGILIA USHINDI WA NIGERIA

Shola
Ombi la kutaka refa Peter O’Leary kuondolewa katika listi ya kuchezesha mechi kwenye michuano ya Kombe la dunia limepata sahihi elfu 20 kutoka kwa mashabiki wa Bosnia kutokana na kitendo alichofanya wakati wa ushindi wa timu ya Nigeria wa goli 1-0.
Hatua hiyo imetokana na picha iliyomuonyesha refa huyo akishangilia ushindi na kumkumbatia golikipa wa timu ya Nigeria Vincent Enyeama.
Mbali na kutaka refa huyo aondolewe kutoka kwenye michuano hiyo, pia mashabiki wanataka matokeo ya mchezo huo kubadilishwa na kuwa 1-1 kumaanisha bado timu yao ipo  katika mashindano.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com