Mauaji Kishapu!! KIJANA AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KUBWA KICHWANI BAADA YA KUWADHULUMU WENZAKE PESA ZA MAUZO YA ALMASI

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la  Mihangwa Maguta (30) mkazi wa kijiji cha Nyenze Matelu kata ya Mwadu- Luhumbo tarafa ya Mondo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ameuawa baada ya kupigwa kwa jiwe kubwa kichwani na watu anaodaiwa kuwadhulumu pesa za mauzo ya madini ya almasi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya tukio hilo limetokea jana (Mei 7,2014) saa moja asubuhi katika kijiji hicho cha Nyenze Matelu wilayani Kishapu.

Imedaiwa chanzo cha mauaji hayo  inasadikiwa  kuwa marehemu  amewadhulumu  wenzake watatu pesa za mauzo ya madini ya almasi.

Tayari jeshi la polisi mkoani Shinyanga  linawashikilia watuhumiwa wa mauaji hayo akiwemo Makoye Manyenze aliyesababisha kifo cha Mihangwa Maguta.

Watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa na polisi ni Abdalah Idd (32) na Ally Omary (22) wote wakiwa ni wakazi wa  kijiji cha Nyenze Matelu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments