MASKINI MUME NA MKE WANUSURIKA KUFA KWA KUUNGUA MOTO,TAZAMA PICHA ZINASIKITISHA,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI



Majeruhi wa kwanza Chacha Wambura (35)akiwa amelazwa katika wodi namba 7 katika wilaya ya Geita baada ya kuungua moto katika kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita mkoani Geita.


Majeruhi wa pili mke Chacha Wambura bi Happiness Chacha (22) akiwa amelazwa katika wodi namba 8 katika hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kuungua moto yeye na mme wake-Picha zote na Valence Robert

Wanandoa  wawili wakazi wa kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita  mkoani Geita Happiness Chacha(22) na mme wake Chacha wambura(35) wamenusurika kufa baada ya nyumba yao kuungua moto katika kibanda chao cha bar.

Tukio hilo limetokea jana usiku saa nane usiku katika kijiji cha Lwamgasa ambapo kufuatia tukio hilo majeruhi wakikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Geita mkoani Geita walipolazwa wodi namba 7 na 8.

 Robina Isack anayewauguza amesema kuwa usiku huo wa saa 8 waliona moto unawaka bila kujua umeanzia wapi huku wakishangaa kwa vile hawatumii nishati hiyo ya umeme na wala hapakuwa na moto waliokuwa wamewasha ndani.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Na Valence Robert wa Malunde1 Blog -Geita


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post