MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI,SHINYANGA YAFANYIKA UWANJA WA KAMBARAGE

Ni katika viwanja vya CCM Kambarage mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani kimkoa.Wa tatu kutoka kulia ni mgeni rasmi katika sherehe hizo kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Annarose Nyamubi  ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga,akiwa katika jukwaa kuu wakati wa kupokea maandamano ya wafanyakazi kutoka mjini Shinyanga kuelekea katika uwanja wa Kambarage.Wa tatu kutoka kushoto ni mwenyekiti wa shirikisho la wafanyakazi mkoa wa Shinyanga Fue Mlindoko.
Miongoni mwa mabango waliyokuwa wamebeba wafanyakazi wa mkoa wa Shinayanga leo katika uwanja wa ccm Kambarage mjini Shinyanga,ambapo pamoja na mambo mengine wafanyakazi hao wamewataka waaajiri kuacha tabia ya kuwanyanyasa na kuwafukuza kama wanyama,lakini pia kuitaka serikali kuwajali wafanyakazi kwa kusimamia sheria ya waajiriwa ya mwaka 2008 kuruhusu wafanyakazi wachague mifuko ya hifadhi ya jamii wanayoitaka mwenyewe bila kulazimishwa na waajiri waa kutokana na baadhi ya mifuko hiyo kushindwa kuwanufaisha wafanyakazi  katika mafao yao kama unavyoona kwenye bango hilo hapo mbele.
 
Picha kwa hisani ya Stella Ibengwe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post