Updates!! HII HAPA NDIYO TAARIFA KAMILI KUHUSU AJALI MBAYA YA BASI KUGONGA NYUMBA NA KUPINDUKA NA KUUA HUKO SIMIYU

Basi la Luhuye likiwa limepinduka baada ya kugonga nyumba  huko simiyu


Watu 11 wamepoteza maisha  papo
hapo na mwingine mmoja kufariki  dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali  ya rufaa ya Bugando,baada ya kutokea ajali mbaya ya gari iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lililokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.

Basi hilo liligonga nyumba kisha kupinduka leo saa tano na dakika 10 asubuhi  katika barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Itwilima kata ya Kiloleli wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Mbali na watu 12 kufariki dunia pia watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa  ni mwendo kasi wa sasi hilo ambapo dereva wa alishindwa kumudu gari hilo likiwa katika kasi na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na kupinduka.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwemo wa malunde1 blog katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amesema miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume 7.

Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kabla ya kutokea kwa ajali  hiyo basi hilo lilianza kuyumba na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa kando kando ya barabara hiyo.

Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Dk Athuman Pembe alithibitisha kupokea majeruhi 60 pamoja na miili 11 ya marehemu.

Amesema kati ya majeruhi hao 25  hali zao siyo nzuri wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, na kwamba hali za majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo zinaendelea vizuri na tayari wengine wameanza kuruhusiwa.

Jeshi la polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post