KUTANA NA SHABIKI WA LIVERPOOL ALIYEFUGA NYWELE ZAKE MIAKA 11,AKIAPA KUTOZIKATA HADI LIVERPOOL IWE BINGWA WA EPL

uka1_9644Shabiki wa mmoja wa klabu ya Liverpool huko nchini Kosovo ameweka kiapo kilichodumu kwa miaka 11 juu ya klabu ya Liverpool.
Shabiki huyo aliyefahamika kwa jina la Ukë Krasniqi aliweka kiapo cha kutokukata nywele zake miaka 11 –  kuanzia mwaka 2003 mpaka leo hii, akiapa kwamba hatozikata nywele hizo mpaka pale Liverpool itakapotwaa ubingwa wa Uingereza maarufu kama Barclays Premier League.
Hivi sasa story hiyo ya raia huyo wa Kosovo imetengeneza headlines na gazeti la Kosovo Republika.mk, limemfanyia mahojiano Ukë Krasniqi na haya ndio aliyosema:
“Tangu mwaka 2003 nilianza kufuga nywele zangu…Mpaka sasa Liverpool imeshinda kila kombe lakini sio Premier League. Sasa tumekaribia kushinda ubingwa huo. 
Hata kama tutangazwa mabingwa mapema, nitaendelea kufuga nywele zangu mpaka May 11. Nataka kushangilia na nywele zangu  wakati Steve Gerrard atakapobeba kombe kwa mara ya kwanza, kisha baada ya hapo nitakata.” 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post