Breaking News!!! AJALI MBAYA,BASI LAUA WATU KIBAO PAPO HAPO BAADA YA KUGONGA NYUMBA KISHA KUPINDUKA HUKO SIMIYU

Habari zilizoufikia mtandao wa Malunde1 blog hivi punde kutoka mkoani Simiyu ni kuhusu ajali mbaya ambapo watu zaidi ya 10 wamefariki dunia papo hapo na wengine wengi kujeruhi baada ya basi la Luhuye walilokuwa wanasafiria kugonga nyumba na kupinduka kutokana na kile kilichotajwa kuwa mwendo kasi wa basi hilo.

Habari zinasema kuwa basi la abiria la kampuni ya Luhuye lenye namba za usajili T 410 AWQ lililokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza limegonga nyumba na kupinduka  leo saa tano asubuhi  katika barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Itwilima kata ya Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post