ASKOFU MDEGELA AWA MBOGO,ASEMA UKAWA WAFUNGE VIRAGO WARUDI NYUMBANI BADALA YA KUENEZA CHUKI KWA WANANCHI,AKEMEA WANAOTUKANA WAASISI WA TAIFA,SOMA NA TAZAMA VIDEO YAKE HAPA

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya  Iringa  Dr.Owdenburg Mdegela
Na  Francis Godwin, Iringa 

ASKOFU mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya  Iringa  Dkt. OwdenburgMdegela ameitumia ibada  ya Jumapili ya Pasaka leo  kulaani vikali  wale wote  wanaowatukana waasisi wa Taifa  hili Sheikh Abeid Amani Karume  na Mwalimu hayati Julius Kambarage Nyerere.

Askofu Dkt  Mdegela amesema kuwa watu hao wanapaswa kuwaomba radhi  watanzania huku akisisitiza wajumbe umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kurejea bungeni ama  kufungasha  virago  vyao na kurudi nyumbani kwao na sio kuzunguka kupandikiza chuki kwa wananchi.

Askofu Dr Mdegela aliyasema hayo leo  wakati akitoa  salam za pasaka kwa  waumini  wa Dayosisi hiyo kupita washarika wa  kanisa  kuu.

Dkt. Mdegela asema "Watanzania tunataka  kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani na  kuanza  kutafuta kuvuruga amani  na utulivu  wetu ambayo ni lulu ya pekee inayogombewa na nchi  nyingine na  kuwa  wanaotaka lulu  hiyo ivurugike wasivumiliwe kamwe.

"Kinachofanywa  bungeni kwa  sasa ni mzaha wa hali ya juu na  Watanzania wanapaswa  kuwachunguza vema  wawakilishi wao hao wakiwemo wabunge wa vyama  vyote na  wale wanaoeneza mbegu ya  chuki  wasichaguliwe tena...."

Asema wajumbe wa bunge la katiba  hawana  sifa ya  kutengeneza katiba kwani  wametanguliza mzaha na matusi  yasiyo na tija  na kuwa hawa  wanaokwepa  bunge na kutaka kuzunguka kwa wananchi  wanapaswa kuzuiwa kufanya  hivyo na vyombo vya usalama kwani wanataka  kuipeleka nchi pabaya.

"Kama wamekula pesa za wananchi kwa muda  wote huo kwa ajili ya kuunda katiba iweje  leo  watoke bungeni na kudai  kuja kwa wananchi mikono mitupu??" amehoji.

"Wananchi tuwakatae wajumbe  wanaotaka  kuzunguka kupandikiza  chuki kwa wananchi kwa kujiita  wao wapo kwa ajili ya katiba ya  wananchi hali  wamekimbia bunge na kutaka  kutuwakilisha nje ya  bunge 

"....tunawakataa  wao na mawazo yao na pia kama wajumbe wa bunge  hilo  wameshindwa kazi tutaikataa rasmu ya katiba ambayo italenga  kutugawa  watanzania.

"Na niweke  wazi mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba mbali ya kazi  hiyo bado tunawajibu wa kumrekebisha pale  alipokosea kwani Wazanzibar wa Pemba wanataka serikali nne sio tatu mbona hajaeleza

" ....nasema serikali mbili ni  jibu kama haiwezekani bado tuwe na serikali moja itakayotuunganisha"

Hata  hivyo Dr Mdegela alisema  kuwa msimamo  wake na waumini  wa kanisa  hilo ni kuwa na serikali mbili na ikiwezekana  kuwa na serikali  moja  pekee na si vinginevyo na iwapo  wajumbe wa  bunge la katiba  wameshindwa kazi na kugeuza  bunge  hilo ni sehemu ya kuonyeshana ujuzi wa kutukanana ni  vema wakirudi katika mwelekeo mzuri ama kurudi majumbani kwao  ili viongozi wa dini mashekhe na maaskofu wakaifanya kazi hiyo ya kuunda katiba  bila kutukanana .
"Nimejizuia  sana kwa kipindi  hiki  cha bunge la katiba  nisiseme  chochote ila  kutokana na mambo jinsi yanavyokwenda uvumilifu  umenishinda nimelazimika  kusema na ninachosema nimekiandika ili  wale  wapotoshaji washindwe  kupotosha ninachosema....wayahudi  walikataa kuongozwa na Samweli kwa  sababu walisema  watoto wa Samweli wanatabia  mbaya ...walikataa kuongozwa na Mungu kwa madai  kuwa na  wao  wanataka mfalme wetu  uli tukienda  kupigana na watu  ili  tuwe kama mataifa  mengine  ila Mungu hakutaka wao  kuwa kama mataifa  mengine  ila  wao  wanataka  kuwa kama mataifa  mengine ....Samweli akaenda mbele ya Mungu akilia ....ila  Mungu akasema hawajakukataa wewe  wamenikataa mimi ...enyi  watanzania tukikataa lulu  tuliyopewa na Mungu ya kuwa nchi ya amani  tutakuwa hakuwakatai viongozi  wetu  tutakuwa tunamkataa Mungu"

Aliwataka  watanzania  kuyatazama mataifa  jirani kama Kenya ambao  walijipenda  wao na kushindwa  kuwapenda  majirani  sasa  Wasomari  wameingia wanawasumbua  ila tazameni pia Malawi ambao walimtaka rais  wao awe Joys Banda ila alipoingia tu Ikulu alitangaza ndoa za jinsia moja pamoja na nchi ya Kongo ambayo imesaidiwa na Tanzania kurudi katika amani ikiwemo nchi ya Burundi  ambayo Rais  wake amekuwa akishinda katika maombi kwenye kanisa lake na kuacha kuongoza nchi.

"Tunapaswa  kujiuliza amani  hii iweje  leo  ichezewe na  watu  wachache  wenye uchu wa madaraka na hata  kususa  bunge la katiba ...hatujifunzi  kutoka nchi  za majirani  zetu kama Uganda ,Rwanda kuna  vyama 10  vya upinzani na kuna  vikundi 10  vinavyotaka  kumpindua Rais huku Uganda kuna mtu anaitwa Kony yeye  siku  zote  kumshumbua Rais ....ninyi ni nani  Tanzania bara  na visiwani mkaa kwenye amani kiasi hiki na mnakataa umoja na kuanza kuwasikiliza  wanaopandikiza mbegu ya kuvuruga amani ya kutaka serikali tatu ....watanzania tunataka  kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani"

Dr Mdegela  alisema kuwa hadi  sasa mwenendo  wa  bunge la katiba unatia aibu kubwa kwa  Taifa na hata nje ya taifa   hili na kuwataka  wajumbe hao  kuwa wasikivu na kama  walisema  wanakwenda kuandaa katiba ya  wananchi iweje kabla ya  kuanza kwa  bunge  hilo walianza kwa kulilia posho kuongezwa hali  wakijua  walimu hawajalipwa malipo yao pamoja na  wafanyakazi  hawajaongezwa mishahara yao.


"Natamka  wazi  kuwa  mimi Dr Mgedela sina  imani hata  kidogo na  wajumbe wa  bunge la katiba .....kama  wanavyoonekana na  walivyo wana hadhi ya kutoridhika  watatuletea  katiba mbovu kwa  sasa na  wao  ni wabovu ..

"Natamka rasmi  kuwa  tume iliyoandaa rasmi ya katiba haukuandaa msaafu  wala Biblia  ili andaa kitu ambacho  mbacho  kinaweza  kuhojika na kukataliwa  ama kukubalika  wao  si Miungu ni  wanadamu kama  sisi madai kuwa wanavyeo vingi  serikalini hata mfagiaji anavyo ....sasa naiomba serikali hao  waliojitoa bungeni wanataka kuja kwa wananchi tunasema hatuwataki ....

"Hivi kama mtu ameshindwa  kujenga  hoja bungeni watakuja kutueleza nini nawaombeni usalama wa Taifa fanyini kazi ya kulinda amani yetu ....kama hawataki kurudi bungeni basi waende majumbani kwao"

Askofu Dr Mdegela  alisema kanuni za bunge  wametunga  wao na iweje leo  wanakimbia kanuni waliyoitunga hivyo kama  wanaona kanuni  ni mbaya  basi  watuombe Watanzania wenye akili tuwasaidie hata   yeye anaweza kwani  wajumbe hao ni walafi  wasiopenda amani ya nchi hii.

Katika  hatua  nyingine  askofu  huyo  alisema kwa  sasa  kinachoendelea na kuwa  kila kanda  itataka  serikali  yao iwapo  hoja  ya  serikali tatu  ikapitishwa.

TAZAMA VIDEO YA ASKOFU MDEGELA AKIZUNGUMZA HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post