NDEGE YA MALAYSIA MH370 ILIANGUKA BAHARI YA HINDI NA KUSABABISHA VIFO VYA ABIRIA WOTE WALIOKUWEMO KATIKA NDEGE HIYO

http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/03/Screen-Shot-2014-03-17-at-11.49.52-PM.png


 
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak.

 
Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak, amesema data mpya zinaonyesha kuwa ndege ya nchi hiyo iliyopotea  imeangukia kusini mwa Bahari ya Hindi. 

Razak amesema taarifa hizo zimeonyesha kuwa eneo la mwisho la ndege hiyo ilikuwa katikati mwa Bahari ya Hindi, magharibi mwa mji wa Perth, Australia. 

Amesema eneo hilo liko ndani ndani na liko mbali na uwanja wowote ule wa ndege.

Amesema kulingana na data hizo mpya, ndege nambari MH 370 iliangukia kusini mwa Bahari ya Hindi. Razak amesema taarifa zaidi kuhusu data hizo mpya, zitatolewa kesho Jumanne.
via>>dw swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post