MTANDAO MPYA WA SIMU ZA MKONONI WAJA BONGO, UNAITWA SMART

Mtandao wa ‘Smart Lets Talk
TAASISI ya Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) kwa kushirikiana na tasisi ya mtandao wa usambazaji wa huduma (IPS network) imeingia katika soko la pamoja la mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki  kwa kuzindua mtandao mpya wa simu za mkononi uitwao Smart.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart, Abdellatif Bouziani, alisema wameamua kuanzisha mtandao huo kwa kutambua changamoto nyingi zinazoikumba sekta ya mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki  na kwamba mtandao huo utarahisisha mawasiliano na kwa gharama nafuu.

“Mtandao wa ‘Smart Lets Talk’ utawawezesha watumiaji wa hali zote kumudu gharama za mawasiliano kwa kuwa mteja ataweza kupiga simu kwa mara ya kwanza hadi atakapokata kwa  shilingi 79,” alisema.
Via>> http://kandorodaddycool.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post