MGEJA AKABIDHI LUNINGA KWENYE KIJIWE CHA KAHAWA CHA BBC KATIKA MJI MDOGO WA ISAKA-KAHAMA

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabdhi Luninga kwa Wajasiliamali wa BBC katika Mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama
Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi  fedha kwa ajili ya kebo ya

TV muda mfupi baada ya kukabidhi Luninga kwa kijiwe cha Kahawa cha BBC katika Mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja jana amekabidhi msaada wa luninga yenye thamani ya shilingi 260,000/= kwenye kijiwe maarufu cha wajasiliamali cha  Kahawa maarufu kwa jina la BBC kilichopo katika mji mdogo wa Isaka Wilayani Kahama wakati akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.

Wajasiriamali hao walimwomba mwenyekiti huyo wa CCM msaada huo wa Luninga ili waweze kupata habari kupitia chombo hicho hasa nyakati za asubuhi na jioni kabla ya kazi na baada ya kazi ili kwenda sambamba na mambo yanatokea ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na wajasiriamali hao baada ya kukabidhi luninga hiyo Mgeja aliwataka wazee na vijana kujenga utamaduni wa kuridhika na vipato vidogo wanavyovipata kulingana na hali waliyonayo badala ya kukimbilia vipato vya juu ambavyo vipo nje ya uwezo wao wa kimahitaji.

Kufuatia msaada huo mwenyekiti wa Wajasilimali hao wa BBC Ally Salumu Msangi alishukuru na kuongeza kuwa msaada huo umefika katika kipindi muafaka hasa wakati wa kipindi hiki cha bunge la katiba linaloendelea mjini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post