AUAWA BAADA YA KUTISHIA KUWAROGA WANANZENGO HUKO KATAVI

NB-Haihusiani na tukio
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Kalenga  Mashaka  52  Mkazi  wa Kijiji  cha Kusi , makazi ya wakimbizi ya MishamoWilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  ameuwawa  kwa kupigwa  na kitu  kizito  kichwani  na watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari   tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa mbili asubuhi kijijini  hapo.
Alisema katika uhai wake marehemu  aliwahi  kufikishwa   mahakama ya mwanzo ya Mishamo  kwa kutuhumiwa  kutishia kuua  kwa maneno ambapo alikuwa  akiwatishia watu  kuwaua  kwa njia ya ushirikina.
Kamanda Kidavashari alifafanua kuwa kitendo hicho cha kuwatishia wakazi wa kijiji  hicho  kwa njia ya ushirikina kilijenga chuki baina ya marehemu na wanakijiji hicho.
Alifafanua kuwa  kwa  mujibu wa uchunguzi wa  awali   chanzo   hicho kutishia   kuwauwa kwa ushirikina wanakijiji wenzake  ndicho kilichosababisha kutokea kwa mauwaji ya mtu hoyo.
Alisema kuwa  wanakijiji  hicho cha Kusi  walikuwa wamechoshwa na vitendo hivyo  vya kutishiwa kuondolewa uhai wao kwa njia ya ushirikina alivyokuwa akivifanya marehemu  Kalenga.
Kidavashari  alieleza  kabla ya tukio la marehemu    kufikishwa  kwenye mahakama ya mwanzo ya Mishamo  wanakijiji hicho  waliwahi kujichukulia   sheria  mkononi  kwa kuichoma moto nyumba ya marehemu  kwa lengo la  kumfukuza kijini hapo.
Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo  ili kuwabaini watu au mtu aliyehusika na mauwaji hayo ili  waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Na  Walter Mguluchuma-Katavi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post