Usiombe kukutana na matapeli!! MAMA WA MAKAMO ALIA KAMA MTOTO BAADA YA KUTAPELIWA MIL 5


Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya Februari 20 mwaka huu.
Bi. Shembusho akilia kwa uchungu baada ya kudangasnywa na watu wawili, wa kike na wakiume ambao majina yao bado hayajafahamika. watu hao walimpeleka katika Hoteli maarufu mjini moshi, Fresh Coach na kumtapeli shilingi milioni 5.4 ambazo alikuwa ametoka kutoa Benki ya Uchumi ya mjini Moshi.Askari wa Hoteli hiyo inayodaiwa kutumika kumtapeli mwanamke huyo akimtuliza Mama huyo ambaye alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo.Mama akilia kwa uchungu.. Keleuwieeeeeee...!!!!!

Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.

Mama akisimulia tukio zima kwa wananchi waliofika katika eneo la tukio baada ya kumsikia akipinga ukunga kuomba msaada.Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.

Na Dixon Busagaga 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post