Ukatili!!! MREMBO ABAKWA KISHA KUNYONGWA HUKO MOROGORO,AKUTWA NA TIKETI YA DSM>>MORO

Dada mmoja anayedaiwa kuwa mkazi wa jijini Dar es Salaam ameuawa kinyama baada ya kubakwa hadi kufa eneo la Nanenane ndani ya mashamba ya mikonge mjini Morogoro.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, mrembo huyo ambaye hakufahamika aliuawa kwa kubakwa na watu wasiojulikana ambapo maiti yake ilikutwa ikiwa imevuliwa nguo za ndani. 
Aidha, kwenye shingo yake kulikutwa na kitambaa ambacho inadhaniwa kuwa ndicho kilichotumika na wahalifu kumnyongea.

 
Baada ya polisi kukagua pochi yake walikuta ikiwa na tiketi iliyoonyesha kuwa alisafiri kutoka Dar es Salaam hadi mjini hapa bila kuwa na jina la msafiri. 
 
Baadhi ya wananchi walioshuhudia maiti hiyo, wamesikitishwa na tukio hilo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustene Shilogile alipohojiwa juzi na mwandishi wetu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. 

“Nawaomba watu wanaomfahamu marehemu huyu wafike chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kumtambua,” alisema Shilogile.
credit-kandili yetu leo 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post