Noma kweli!! SISTA DUU ATOROKA HOSPITALI,AKIKWEPA KULIPIA MATIBABU ,ALIANZA KWA KUGAWA NGUO ZAKE KWA KILA NDUGU ALIYEFIKA KUMSALIMIA HOSPITALI

Watu kibao na wagonjwa  wamejikuta wakibaki midomo wazi,baada ya mgonjwa mmoja ambaye jina lake linalihifadhiwa ambaye alikuwa amelazwa hospitali moja huko Kampala Uganda kutoroka hospitalini hapo pasipo na kulipa pesa ya matibabu pamoja na malazi..

 Inadaiwa kuwa dada huyo alifika hospitali hapo akiwa yuko hoi hajitambui kufuatia kupata ajali ya pikipiki maarufu kama bodaboda hivyo kulazimika kukaa hospitali hapo karibia mwezi mzima.. 

Walioshuhudia tukio hilo walisema mtuhumiwa huyo alianza kukabidhi nguo zake kwa ndugu zake kila walipokuja kumuona .. na ndipo jioni alipooga na kuvaa kisista duu na kuondoka huku akiwaaga wagonjwa wengine kwamba anaenda kufanya mazoezi ya kutembea tembea.

 Karibia masaa matatu yakapita  bila dada huyo kurejea na ndipo dokta alipokuja kumdischarge na kukuta kitanda kitupu...

Akizungumzia tukio hilo  mama mmoja ambaye anadai mara nyingi ana bahati ya kulazwa mara nyingi na dada huyo amedai ndiyo tabia yake na inabidi kusambaza picha zake kila hospitali hili asiendelee kutia hasara kwa kutapeli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post