MWIGIZAJI SHAMSA FORD AUGUA KICHAAMwigizaji wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na mtoto wake wakiburudika.


Stori:SHANI RAMADHAN MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa aliwahi kuugua ukichaa.

Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Shamsa alisema ukichaa huo aliupata alipokuwa akisoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kunduchi-Beach, jijini Dar ambapo alilazimika kukaa nyumbani kwa takriban mwaka mzima kupatiwa matibabu.


Akifafanua zaidi kuhusiana na ugonjwa huo, mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, alisema ulimtokea ghafla, alijikuta ameanza kushikashika vitu hovyo, kuzungumza maneno yasiyoeleweka ndipo wazazi wake walipoamini amepatwa na tatizo la akili.

Alipelekwa hospitali na kupewa dawa za kutumia na zaidi anamshukuru Mungu, mama yake ni mshikadini, kwani alimuuombea hadi akapona na kuendelea na masomo kwa kurudia kidato cha pili.

“Nilikuwa ni mtu wa kuhangaika mara huku mara kule, yani naongea vitu ambavyo havipo, lakini namshukuru sana Mungu alinisaidia baada ya kuzunguka sana na mama pamoja na ndugu zangu waliokuwa wakiniombea dua, nilipona kabisa,” alisema Shamsa.

Kuna wakati akiwa katika hali hiyo, Shamsa alifikia hatua ya kujisaidia haja zote bila kuvua nguo.

“Akili haikuwa yangu, niliweza kufanya kitu ambacho nilikatazwa, nilikuwa nikirudia mpaka nikawa nalindwa, sikuachwa peke yangu hata dakika moja” alisema staa huyo ambaye yuko katika mchakato wa kufunga pingu za maisha na mzazi mwenzake, Dick.

SOURCE: GPL

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post