
Mtoto Tatu Hassan akiwa mwenye furaha na mama yake mzazi Bi. Halima Mgelwa, mtoto huyu amekuwa kitandani kwa zaidi ya miaka kumi na moja kutokana na maradhi ya kichwa kujaa maji huko katika kijiji cha Magiri wilayani Uyui mkoani Tabora.

Mama wa mtoto huyu anaomba msaada wa matibabu kwa wasamalia wema,tatizo kubwa kichwa cha mtoto huyu kimejaa maji na hivyo anahitajika kupelekwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Mama huyu kwa mujibu wa maelezo yake amekuwa akilazimika kumfungia ndani ya nyumba kila siku na kwenda kutafuta riziki kwa muda wote huo wa miaka kumi na moja na hivyo hata baadhi ya majirani zake wa karibu hawatambui kama kuna mtoto huyu hapo kijijini.
Jambo baya zaidi baadhi ya watu wenye imani potofu walithubutu kumshawishi mama huyu aweze kumpa SUMU mtoto wake eti kwa madai kwamba amekuwa akihangaika sana kumuhudumia
Credit-Eddy blog
Post a Comment