Inasikitisha sana!! DEREVA WA LORI LA MAFUTA ATEKETEA KWA MOTO KATIKA AJALI HUKO MOROGORO

Baadhi ya watu waliokwama kijiji cha Fulwe kata ya Mikese mkoani Morogoro wakiangalia mwili wa dereva wa lori lililobeba shehena ya mafuta lililokuwa likitoka Dar kueleka upande wa Morogoro, ukiwa umeteketea vibaya kwa moto baada ya ajali.
 
Mwili Mwili wa dereva wa lori la mafuta ukiwa umeteketea kwa moto.
Lori la mafuta baada ya kuteketea kwa moto kijiji cha Fulwe, Mikese mkoani Morogoro.
AJALI hii imetokea leo katika kijiji cha Fulwe, kata ya Mikese mkoani Morogoro ambapo malori mawili yamegongana na kuteketea kwa moto.

Katika ajali hiyo, dereva wa lori moja lililokuwa na shehena ya mafuta amepoteza maisha wakati dereva wa lori lingine aina ya semitrela akijeruhiwa pamoja na tingo wake na kukimbizwa hospitali.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo amedai kuwa dereva aliyepoteza maisha alishindwa kujiokoa baada ya ajali kutokea kwa kubanwa hali iliyopelekea kuungua vibaya kwa moto.

"Lori hili la mafuta lilikuwa likitoka Dar na kushuka mteremeko huu kwa kasi huku semitrela likijaribu kulipita lori lingine eneo hili hivyo kugongana uso kwa na lori la mafuta.

Baada ya kugongana, mafuta yaliokuwa kwenye tenki yalimwagika hali iliyosababisha malori yote kuteketea kwa moto. " Alisema shuhuda huyo mkazi wa kijiji cha Fulwe, Bw Issa Athuman.
Credit-GPL

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post